Thursday, February 6, 2014

SEMINA YA KUFUNGA VIZURI: SIKU YA PILI

FAIDA MBALIMBALI TUNAZOPATA KUTOKANA NA KUFUNGA VIZURI.
Semina ya kufunga vizuri imeendelea leo katika kanisa la BMCC. mchungaji amekazia sana juu ya faida zinazo tokana na kufunga vizuri.
1. Funga inatuwezesha sisi kuisikizisha sauti zetu kwa Mungu
2. Nuru yako itapambazuka. maanayake funga inakupa kibali cha huduma zingine.
3. Afya yako inatokea. Funga inaleta uponyaji. funga nidawa ya kutokuzeeka Kumbukumbu 34:7
4. Funga inakuwezesha kupata haja yako bila wewe kuombewa. haki yako itakutangulia.
5. Utukufu wa Bwana utakufuata nyuma ukulinde. funga inaleta ulinzi
6. Funga inamwezesha mfungaji kila anapoita ajibiwe na Bwana.
7. Machozi ya mtu aliyefunga ni uwepo wa Bwana
8. Funga inatuongoza sisi tutembee sawa sawa na mapenzi ya Mungu
9. Funga inatuwezesha kuhamisha mikosi kutoka kwako kwenda kwa watoto wako, na watoto wakiomba mikosi inaenda kwa wajukuu, hivo hivo. Zab35:13, Yer36:6

SIKU ZA KUFUNGA NA FAIDA ZAKE.
Faida za kufunga siku moja
1. Utajua mapenzi ya Mungu
2. Mungu huleta ulinzi juu yako. Ezra8:21-23
Faida ya kufunga na kuomba siku tatu kavu.
1. Utapata kibali Ester4:16
Funga ya siku 21
1. Hii nifunga yakuongeza maalifa ya kimungu.
Funga ya siku 40
Hii nifunga ya utawala, walifunga Musa, Elia na Yesu.
1. Funga hii inakupa kibali cha huduma
2. Mtu anayefunga mfungo huu, hata kifo chake kinakuwa cha utukufu. Angalia kifo cha Musa, Eliya na Yesu. watu watasema kweli huyu alikuwa mtumishi wa Mungu.
3. Udhihilisho wa nguvu za Mungu sana unawahusisha watu wanaofunga siku 40. Angalia wakati Yesu alipokuwa na wanafunzi wake, wakina Petro, mlimani, ghafla wingu liliposhuka, Musa na Eliya wakaokea.
Semina itaendelea kesho endelea kufuatilia. Ubari
kiwe



No comments:

Post a Comment