Wednesday, February 5, 2014

SEMINA: JINSI YA KUFUNGA VIZURI BY PASTOR ONAEL E. MDOBILU (SEMINAR ON GOOD FASTING)

Semina ya siku tano imeanza leo katika kanisa la Beacon Mission Christian Center, Mchungaji Onael E.Mdobilu kutoka TAG-Manzese anafundisha.
Kamasehemu ya utangulizi, ameanza kufundisha jinsi ya kufunga vizuri. katika maneno yake ya awali, amesema kwamba ni muhimu tuombe kama kanisa kwani Tanzania tuliyo nayo sasa sikama ya zamani, wakati huu taifa linategemea sana maombi ya kanisa.
Amesema pia kuomba mara zote hakupotezi muda bali hukomboa Muda, mambo ambayo ungeya hangaikia kwa muda hata wa miaka 30 baada ya maombi yenye nguvu unaweza ukajibiwa kwa haraka.
vitabu vya msingi ni: Mathayo 17:14-21, Waamzi :20:17-26, 35, Isaya 58:3-11
Kufunga kunauleta uwepo wa Bwana, ukiacha kula ukafunga hali yako ya kiroho inabadilika. Lakini msingi wa kufunga nikuisikizisha sauti yako juu, kufunga haipaswi kuwa mashindano, wala kila mtu ajue. maanayeke, funga kwa ajili ya BWANA Mungu aonaye silini atakujibu.

MAMBO NANE ILI UFUNGE VIZURI
Ili ufunge vizuri, ili Mungu aikulabili saumu yako kuna mambo nane lazima ufanye ukiwa umefunga
1. Kufungua vifungo vya uovu
2. Kuzi legeza kamba za nira
3. Kuwa acha huru walio onewa
4. Kuvunja kamba za nira
5. Kuwa gawia wenye njaa chakula chako
6. Kuwaleta masikini walio tupwa inje nyumbani kwako
7. kuwavika nguo walio uchi
8. Usijifiche na mtu mwenye damu na wewe aendelee dhambini.(usimwache ndugu yako aendele dhamini, maana yake muombee ndugu yako ambaye amefungwa na dhambi)

Maana yake funga yakweli inayopata kibali kwa Mungu ni ile unayotumia kuomba kwaajili ya kuwaleta watu kwa Yesu, kumkemea shetani aachie maisha ya watu. Dhambi ni nira ambyo humufunga mtu. kwa hiyo kufunga kunaleta upako ambao Mungu anataka utumie kuvunja nira.

AINA MBALIMBALI ZA KUFUNGA
Mtumishi amehitimisha leo kwakufundisha aina mbali mbali za kufunga, kuna aina 12 za kufunga
1. Funga yakuvusha mlo mmoja, unaacha mlo mmoja kwa siku.
2. Funga ya kuvusha milo miwili
3. Funga ya kuvusha milo mitatu. au kavu sku moja
4. Funga ya kuvusha milo sita au kavu siku mbili (masaa48)
5. Funga ya kuvusha milo tisa au kavu siku tatu
6. Funga ya kuvusha milo 12 au kavu siku inne. Hii tunaita supper natural fasting, kwa sababu mwanadamu kwa hali ya kawaida anauwezo wa kufunga siku tatu kavu, zaidi ya hayo unahitaji uongozi wa Roho mtakatifu.
7. Funga ya maji tu (water fasting)
8. Funga y maji maji tu (Liquid fasting). hapa unaweza kunywa maji juice na soft drinks zote
9. Funga ya Daniel. Daniel alifunga kwa kula chakula kisicho kitamu
10. Funga ya Yohana mbatizaji. Yohana alikula Nzige na asali.
11. Funga ya kulazimishwa. 1samwel 30:11-13
12. Funga ya hadhala. Funga ya Yona


Maana yake funga zote ni sili, sio kila mtu ajue. isipokuwa funga ile ya Yona ambayo kilamtu alijua.
Tunafunga kwa ajili ya Mungu si kwakujionyesha kwa watu. Amen!

MUNGU AKUBARIKI NA ENDELEA KUFUTILA MAFUNDISHO HAYA.
1 comment:

  1. thank you very much for a nice word. I would real like to learn more about good fasting. Its very true for a person to learn and know a good way of fasting that will draw the attention and receive the answer sooner rather than wasting time. Pastor be blessed and may God keep revealing new things so we may learn and grow in CHRIST. Am blessed with the sermon,

    so where will it be easy for me to get new sermons?

    ...............Blessings...............

    ReplyDelete