Thursday, January 23, 2014

TANGAZO LA KAZI



TANGAZO LA KAZI
Kanisa la Tanzania Assemblies of God – Beacon Mission Christian Centre (BMCC) linatarajia kuanzisha hivi karibuni kituo cha kumhudumia mtoto; hivyo kanisa linatangaza nafasi za kazi kwa watu wote wenye sifa na mzigo na huduma hiyo. Nafasi hizo ni kama zilivyoainishwa hapa chini:
1.    Mkurugenzi wa Kituo (Nafasi moja)
Sifa mwombaji
·         Awe na ujuzi mmojawapo kati ya fani zifuatazo: Watoto na maendeleo yao, Maendeleo ya jamii, Usimamizi wa miradi, Uongozi, Uhamasishaji wa rasilimali, Ualimu, Thiolojia, na fani nyingine zinazofanana na hizi.
·         Awe na elimu, angalau shahada ya kwanza katika fani zilizotajwa hapo juu.
·         Awe Mkristo aliyeokoka na kujitoa kwa Bwana Yesu; mwenye maisha yenye ushuhuda ya kila siku.
·         Awe mwenye moyo wa kujitoa, kutumika kanisani na mpenda maendeleo.
·         Awe na umri kuanzia miaka 25 na si zaidi ya miaka 40.

2.    Mtendakazi wa Jamii (Nafasi moja)
Sifa mwombaji
·         Awe na elimu, angalau Stashahada katika fani zifuatazi: Maendeleo ya jamii, afya ya jamii, Maendeleo ya watoto, Ualimu, na kozi yeyote inayoendana na majukumu yake ya kila siku.
·         Awe mwenye moyo wa kufanya kazi kanisani na kuwatumikia watoto/vijana wahitaji.
·         Awe mwenye maisha ya ushuhuda ya kila siku na wakili wa watoto/vijana.
·         Awe na umri kuanzia miaka 25 na si zaidi ya miaka 40.


3.    Mtendakazi Mhasibu (Nafasi moja)
Sifa mwombaji
·         Awe na elimu, angalau Stashahada katika mambo ya Uhasibu, Manunuzi, au Biashara.
·         Awe mwenye moyo wa kufanya kazi kanisani na kuwatumikia watoto/vijana wahitaji.
·         Awe mwenye maisha ya ushuhuda ya kila siku na wakili wa watoto/vijana.
·         Awe na umri kuanzia miaka 25 na si zaidi ya miaka 40.

Zingatia
·         Maombi yatumwe kwa e-mail, posta au wasilishwe kwa mkono kwa:
Mchungaji Kiongozi
TAG-BMCC
S.L.P 4031
Nyegezi - Mwanza 
Tanzania.

·         Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni Alhamisi tarehe 30/1/2014 saa 5:00 asubuhi.
·         Usaili utafanyika Jumamosi tarehe 1/2/2014 kuanzia saa 2:00 asubuhi katika kanisa la TAG-BMCC.
·         Watakaokuwa na vigezo sahihi (shortlisted) kwa ajili ya usaili watafahamishwa na uongozi wa kanisa kwa njia ya simu tarehe 30/1/2014.

Tangazo hili limetolewa na:
Mch. Valentine F. Mbuke              
Mchungaji Kiongozi (TAG-BMCC)

No comments:

Post a Comment